1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waandamanaji mjini Beijing wameushambulia ubalozi wa Japan na biashara zinazomilikiwa na Wajapan jana Jumamosi, wakitupa mawe na kuvunja madirisha.

10 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFOn

Beijing. Waandamanaji wavunja madirisha ya benki na mgahawa wa Wajapani mjini Beijing.

Ghasia hizo zimetokea wakati wa maandamano dhidi ya juhudi za Japan za kutaka kuonesha kuwa haikufanya uhalifu wowote wakati wa vita vikuu vya pili vya dunia pamoja na nia ya Japan ya kutaka kuwa na kiti cha kudumu katika baraza la usalama la umoja wa mataifa.. Wakati waandamanaji wakipita karibu na mgahawa wa Kijapani , waandamanaji kadha walitupa chupa na mawe na baadaye walilishambulia tawi la benki ya Tokyo Mitsubishi. China hivi karibuni iliishutumu Japan kwa kuidhinisha kitabu cha shule ambacho wakosoaji wanasema kinajaribu kuondoa makosa yote yaliyotendwa na Japan katika vita vikuu vya pili vya dunia.