Waandamanaji Georgia wakabiliana na polisi
30 Novemba 2024Matangazo
Polisi walitumia mabomba ya maji kutawanya umati, na makabiliano yalizuka katika miji ya Tbilisi na Batumi, ambapo waandamanaji walijaribu kuvunja milango ya bunge na kujenga vizuizi.
Ghasia hizo zinafuatia uchaguzi wenye utata uliofanyika Oktoba 26, ambao ulionekana kama kura ya maoni juu ya uanachama wa Umoja wa Ulaya, na kusababisha maandamano ya upinzani na kususia bunge, huku kukiwa na madai kwamba chama tawala cha Georgian Dream kilighushi uchaguzi huo kwa ushawishi wa Urusi.
Rais Salome Zourabichvili alijiunga na waandamanaji Alhamisi baada ya kuishutumu serikali kwa kutangaza "vita" dhidi ya watu wake yenyewe. Katika hotuba yake ya Ijumaa kwa taifa, Zourabichvili aliwasihi polisi wasitumie nguvu dhidi ya waandamanaji.