1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoUfaransa

Waandalizi wa Olimpiki Paris wasema wako tayari kwa Michezo

22 Julai 2024

Rais wa kamati ya maandalizi ya Olimpiki ya Paris Tony Estanguet amesema kuwa mji huo uko tayari kwa Michezo hiyo huku akipuuza malalamiko kutoka kwa baadhi ya wakaazi na wafanyabiashara kuhusu athari za tamasha hilo.

https://p.dw.com/p/4iZKh

Sherehe ya ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki itafanyika Ijumaa ijayo. Matayarisho ya mwisho mwisho yanafanywa katika maeneo yote yatakayotumika kwa michezo hiyo na maelfu ya wanamichezo na maafisa wanamiminika mjini humo. Katika habari nyingine njema kwa waandalizi, ubora wa maji katika Mto Seine -- ambao utatumiwa kwa mashindano ya nje ya uogeleaji katika Olimpiki -- pia umeimarika pakubwa tangu mapema Julai.

Soma pia: Makundi ya Haki za Olimpiki yamsihi rais wa IOC kuondoa marufuku ya hijab

Operesheni kubwa ya usalama kwa ajili ya hafla ya ufunguzi wa Michezo hiyo inasababisha msuguano, huku sehemu kubwa za katikati ya Paris kwenye kingo za mto huo na karibu na viwanja vya Olimpiki zikifungwa kwa umma.

Soma pia:Wanariadha wa Urusi, Belarus kutoshiriki ufunguzi olimpiki

Vyama vya wafanyabiashara vinavyowakilisha maduka ya Paris, migahawa, mabaa na vilabu vimelalamika kuwa vinakabiliwa kudodora kwa biashara, vikilaumu kwa sehemu hatua kali za usalama zilizowekwa.