Wamiliki wa vyombo vya habari nchini Uganda wanaitaka Tume ya Uchaguzi kuhakikisha kuwa vyombo vya usalama havitatizi shughuli zao katika kipindi cha kampeni za uchaguzi wa mwaka 2021. Wito huo ni baada ya tume kutoa mwongozo kwamba kampeni za kisiasa zitaendeshwa kupitia redio na televisheni, vyombo vya habari vinahofia kuwa vyombo vya usalama vitawanyanyasa. Sikiliza ripoti ya Lubega Emmanuel.