1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa waandamanaji wakutana na serikali Ecuador

23 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CEiX

Quito:

Viongozi wa waandamanaji kutoka majimbo mawili yenye utajiri wa mafuta ya Amazon nchini Ecuador, ambako maandamano yalioambatana na ghasia yalizuwia utoaji mafuta wiki iliopita, wameanza majadiliano na serikali ya Rais Alfredo Palacio katika mji mkuu Quito.

Ujumbe wa viongozi wapatao 50 wa waandamanaji, wakiwemo mameya na magavana kutoka mikoa ya Orellana na Sucumbios, watajadiliana na maafisa wa serikali juu ya madai yao kutaka makampuni ya mafuta yatiwe nafasi zaidi za ajira kwa wakaazi wa mikoa hiyo na kuzipatia serikali za mikoa kodi ya mapato na sehemu ya faida ya mafuta yenyewe.

Mazungumzo hayo yanaendelea leo baada ya kuvunjika jana alasiri, pale Meya wa El Coca mji mkuu wa mkoa wa Orellana Ana Rivas, alipotoka kwa hasira, akilishutumu jeshi kwa kukiuka mapatano ya kusitisha mapambano, wakati walöipofyatulia waandamanaji hewa ya kutoa machozi katika mji huo, ulioko kilomita 180, mashariki mwa mji mkuu wa Eduador-Quito.