1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa Umoja wa Ulaya waendelea na Mkutano wao Brussels

30 Juni 2023

Poland na Hungary zimeendelea kupinga mipango inayolenga kusamabaza wahamiaji katika Umoja wa Ulaya kwa haki zaidi, na kutishia kupuuza zaidi juhudi za viongozi wa Umoja wa Ulaya.

https://p.dw.com/p/4TGsl
Belgien I EU Summit
Picha: Ludovic Marin/AFP/Getty Images

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wameingia katika siku ya pili na ya mwisho ya mkutano wao wa kilele mjini Brussels nchini Ubelgiji, ambapo miongoni mwa mambo mengine, wanajadiliana kuhusu mpango wa mageuzi ya sheria za waomba hifadhi wanaowasili katika Umoja huo.

Poland na Hungary zinapinga vikali mabadiliko hayo yaliyokwama kwa muda mrefu. Mabadiliko hayo yanazitaka nchi za Umoja wa Ulaya kugawana waomba hifadhi na nchi zitakazokataa kufanya hivyo zitapaswa kuzilipa fidia kwa nchi zitakazowachukua wahamiaji hao.

Aidha, viongozi hao wa Umoja wa Ulaya watajadili namna ya kupunguza utegemezi wa mataifa yao kwa China, huku wakijadili pia namna ya kuweka usawa na kupunguza hatari katika masuala mbalimbali kama vile mabadiliko ya tabianchi.