Viongozi wa dunia, akiwemo rais wa shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani, Frank-Walter Steinmeier, ni miongoni mwa waliotoa heshima zao mwisho kwa rais wa zamani wa Ufaransa Jacques Chirac, aliyefariki dunia wiki iliyopita. Misa ya kuagwa kwake ilifanyika katika kanisa la Saint Sulpice mjini Paris, Ufaransa. #kurunzi