1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Viongozi vigogo wa chama cha Imran Khan wakamatwa

10 Septemba 2024

Polisi ya Pakistani imewakamata viongozi wa ngazi ya juu wa chama cha waziri mkuu wa zamani aliye gerezani Imran Khan jana Jumatatu.

https://p.dw.com/p/4kRVU
Mkusanyiko wa kushinikiza Imran Khan aachiwe huru
Mkusanyiko wa kushinikiza Imran Khan aachiwe huru. Picha: FAROOQ NAEEM/AFP/Getty Images

Kukamatwa kwao kumejiri siku moja baada ya polisi kukabiliana na wafuasi wa chama cha Khan waliokusanyika mjini Islamabad kushinikiza mwanasiasa huyo aachiwe kutoka gerezani.

Miongoni mwa waliokamatwa kwa tuhuma za uchochezi ni rais wa chama hicho cha Tehreek-e-Insaf, Gohar Khan, ambaye hana mahusiano yoyote ya kidugu na waziri huyo mkuu wa zamani.

Mikanda ya video iliyosambaa mitandaoni imeonesha polisi wakimshusha kiongozi huyo wa chama kutoka kwenye gari lake na kuondoka naye kwenda kituoni.

Chama cha Khan kimesema maafisa wengine wakuu wa chama wamekamatwa kwenye msako wa polisi unaoendelea. Hata hivyo taarifa ya chama hicho haijatoa idadi kamili ya viongozi wake wanaoshikiliwa.

Khan, mpinzani mkuu wa Waziri Mkuu wa sasa wa Pakistan, Shebaz Sharif, yuko gerezani kwa zaidi ya mwaka mmoja kutokana na zaidi ya kesi 150 zilizofunguliwa na mamlaka za nchi hiyo.