Viongozi mafisadi washtakiwa Kenya
3 Julai 2018Mwanasheria mkuu wa Kenya Noordin Mohammed Haji amesema kuna ushahidi wa kutosha uliowasilishwa na tume ya kitaifa ya kupambana na ufisadi unaomhusisha Gavana wa Kaunti ya Busia, Sospeter Ojaamong na ufisadi wa kutumia vibaya ofisi yake pamoja na kula njama ya kutaka kuiba mamilioni ya fedha za umma. Ni mwanasiasa wa kwanza wa cheo cha gavana kuchukuliwa hatua hii katika kesi inayohusisha tuhuma za kutumia fedha nyingi katika miradi ya umma ambayo haijawahi kukamilishwa.
Je, ni kusema sasa serikali ya Kenya imedhamiria kweli kupambana na rushwa, na wanasemaje wachambuzi na wataalamu katika vita dhidi ya rushwa? Saumu Mwasimba amezungumza na mchambuzi na aliyewahi wakati mmoja kuwa mkuu wa tume ya kitaifa ya kupambana na rushwa, Profesa Patrick Lumumba, na alikuwa na mtazamo huu.