Viongozi kadhaa wa Chadema watiwa hatiani nchini Tanzania
10 Machi 2020Uamuzi huo umetolewa na hakimu mkuu mkaazi wa mahakama hiyo, Thomas Simba, baada ya kupitia ushahidi wa upande wa mashtaka na utetezi.
Baada ya kutiwa hatiani viongozi hao wameamuliwa kulipa kiasi cha fedha kinachofikia milioni 340 katika makosa yote, kiwango cha fedha ambacho kinajumuisha washtakiwa wote nane.
Miongoni mwa makosa yaliyokuwa yakiwakabili na hatimaye kukutwa na hatia ni pamoja na lile linalohusiana na uchochezi, kufanya maandamano kinyume cha sheria na kutoa matamshi yenye hisia za chuki.
Baada ya kutolewa kwa fainin hiyo, eneo la viwanja vya Kisutu lilishuhudia umati mkubwa wa wafuasi wa chadema ambao walionekana kushangiliwa jambo ambalo liliwalazimu akari polisi kuingilia kati na kuwaamuru kuondoka mara moja.
Baadhi ya wanasiasa wasema kesi hiyo ingemalizwa kwa maridhiano ya kisiasa
Kumekuwa na maoni tofauti yayoendelea kutolewa kuhusiana na faini hiyo ya milioni 340, na miongoni walioizungumzia ni mwenyekiti wa chama cha NCCR Mageuzi aliyesema kuwa suala hilo lingemalizwa kwa maridhiano ya kisiaasa.
Kwa upande wake, makamu mwenyekiti wa chadema kutoka Visiwani Zanzibar, Saidi Issa Mohemmed alikuwa na haya ya kusema wakati alipohijiwa na idhaaa hii.
"Na kwa kiwango fulani tunasema imejaribu kwahivyo tuchukue fursa hii kumshukuru kwanza mwenyezi mungu kuwashukuru wanachama kumshurkuru jaji kwa angalau kwa hatua ambazo amezifikia," alisema Saidi Issa Mohemmed
Washtakiwa hao ambao bado wanashikiliwa hadi pale watakapomaliza kulipa faini hiyo, walisomewa mashtaka yao kwa mara ya kwanza, mwaka 2018 siku chache tu baada ya kutokea vurugu katika uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Temekeambalo aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo alikihama chama cha CUf na kujiunga na chama tawala CCM.
Mbali ya kuhudhuria na wanasiasa kadhaa wa chama hicho cha upinzani, pia wanasiasa wengine wa upinzani walijitokeza kusikiliza kukumu hiyo. Mbali ya James Mbatia wa NCCR Mageuzi, Mshauri mkuu wa chama cha ACT Wazalendo, Maalim Seif naye alikuwa miongoni mw awanasiasa hao.
Chanzo: George Njogopa DW Dar es Salaam