Kwenye makala ya Vijana Mchakamchaka, Amina Abubakar anazungumza na vijana kutaka kujua ni kwa nini baadhi yao wanazimia raba kali za kisasa, au sneakers, ama kama vijana wenyewe wanavyoziita ''raba za kijanja''. Au ni kwanini vijana wana uraibu wa viatu vya aina hiyo tena vya bei. Je wanajisikiaje wanapovaa raba hizi na wanatafuta nini hasaa wanapovinunua?