1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiNigeria

Vijana wakamatwa kwa kuhudhuria 'harusi ya mashoga' Nigeria

21 Desemba 2022

Polisi wa kusimamia sheria ya Kiislamu katika mji wa kaskazini mwa Nigeria wa Kano wamewakamata vijana 19 kwa kuandaa harusi ya watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja.

https://p.dw.com/p/4LH42
Philippinen | Pride march -  Hände berühren sich
Picha: TED ALJIBE/AFP/Getty Images

Kano ni miongoni mwa majimbo kumi na mawili yenye Waislamu wengi kaskazini mwa Nigeria ambapo sheria kali za Kiislamu zinatekelezwa sambamba na sheria za nchi.

Kwa mujibu wa sheria hiyo kali ya kiislamu, ushoga unaadhibiwa kwa hukumu ya kifo ingawa hukumu hiyo haijawahi kutekelezwa nchini humo.

Mnamo mwaka 2014, Nigeria ilipitisha sheria inayoharamisha ndoa za watu wa jinsia moja na sheria hiyo inaagiza kifungo cha hadi miaka 14 jela kwa yeyote aliyethibitishwa kuwa katika mahusiano ya jinsia moja.