1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VIENNA:Mkutano mkuu wa IAEA kufunguliwa leo

18 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDBH

Shirika la kimataifa la kudhibiti technologia ya Nuklia IAEA leo linafungua mkutano wake mkuu wa 50 unaofanyika kila mwaka.Mojawapo ya ajenda kuu ni suala la Iran.

Nchi 140 wanachama wa shirika hilo zinakutana kwenye mkutano huo mjini Vienna ambapo pia kutakuwepo na warsha ya siku tatu juu ya kutafuta njia ya kuyawezesha mataifa kupata mafuta ya Nuklia kwa ili kujipatia technologia hiyo kwa ajili ya matumizi ya amani na wala sio ya kuwezesha kujitengenezea mabomu.

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani bwana Frank Walter Steinmeier amependekeza kuundwe vituo vya kurutubishia madini ya Uranium chini ya uangalizi wa Umoja wa mataifa ili kuitatua mizozo ya kinuklia kama ule unaoihusu Iran hivi sasa.

Bwana Steinmeier amesema vituo kama hivyo vinaweza kutumiwa na mataifa mengi na kuwekwa chini ya usimamizi wa shirika la kimataifa la kudhibiti technologia ya Kinuklia IAEA.