1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VIENNA: Shirika la nishati ya kinyuklia la Umoja wa Mataifa IAEA limekubalia azimio...

26 Novemba 2003
https://p.dw.com/p/CFxc

likisikitika mno kuwa kwa muda wa miaka 18, Iran imekuwa ikiuficha mapngo wake wa kusafisha madini ya Uranium na kuitengeneza upya Plutonium. Mkuu wa Shirika hilo, Mohammed El Baradei, alisema azimio limetuma risala kali kwa Iran, na inatakiwa kutekeleza masharti ya kimataifa kuhusu mpango wake wa kinyuklia. Wakati huo huo huo, azimio pia linakaribisha chanzo cha Iran kutaka kishirikiana kwa dhati na kwa njia wazi na shirika hilo. Iran imekubalia kuenelezea dhahiri-shahir shughuili zake zote zilizopita za kinyuklia, na iruhusu kukaguliwa barabara vinu vyake vya kinyuklia, na isimamishe harakati za kusafisha madini ya Uranium.