1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Venuezela: Maduro akataa msaada wa kibinadamu

9 Februari 2019

"Sisi siyo ombaomba wa yeyote," Maduro amesema wakati bidhaa za mahitaji zikilimbikizwa kwenye mpaka wa Colombia. Amekataa pia miito kutoka Ulaya na Amerika kuitisha uchaguzi mpya.

https://p.dw.com/p/3D2yX
Venezuela Caracas Nicolas Maduro
Picha: Getty Images/AFP/F. Parra

Rais wa Venezuela Nicolas Maduro amesema Ijumaa kwamba hatoruhusu misaada "bandia" ya kibinadamu kuingia nchini mwake. Misafara ya chakula na dawa vilivyotolewa na Marekani kwa ombi la kiongozi aliejitangaza mwenyewe kuwa rais wa mpito Juan Guaido, imeletwa kwenye mpaka wa Venezuela na Colombia.

"Venezuela haitoruhusu kioja cha misaada bandia ya kibinadamu kwa sababu sisi siyo ombaomba wa mtu yeyote," alisema Rais wa Venezuela, licha ya ushahidi kwamba watu wengi nchini Venezuela wanashinda na njaa kutokana na  uhaba wa chakula. Watu nchini humo wameanza kuelezea ukosefu wao wa chakula kama "lishe ya Maduro," na wamemkabilia hadharani kuhusu hili.

Taifa halikabiliwi na mgogoro wa kibinadamu uliobuniwa na Washington katika kipindi cha miaka minne iliyopita ili kuhalalisha uingiliaji katika taifa letu," Maduro aliongeza.

Alisema msaada unapaswa kutolewakwa maskini katika mji wa Cucuta nchini Colombia, ambako ugavi huo unalimbikizwa. Guaido aliliambia shirika la habari la AFP kuwa atafanya "kila kitu kinachohitajika... kuokoa maisha ya watu," akionya kuwa watu 300,000 huneda wakafariki ikiwa msaada hautaruhusiwa kuingia Venezuela.

Kolumbien, Cucuta: Humanitäre Hilfe aus den USA für Venezuela
Malori ya msaada yakisubiri kwenye mpaka kati ya Venezuela na Colombia, tarehe 8.02.2019.Picha: Getty Images/AFP/E. Estupinan

Akizungumza katika chuo kikuu cha Central Ijumaa, Guaido alisema ni suala tu la muda kabla ya utawala wa Maduro kuanguka: "Tutaendelea kusonga mbele hadi tufanikishe lengo letu," alisema. "Kila siku wanazidi kuwa peke yao na kutengwa." Kiongozi huyo wa upinzani ametambuliwa na mataifa zaidi ya 40, yakiwemo Marekani, Canada, Brazil, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani.

Maduro akataa miito ya kimataifa

Maduro pia amekataa taarifa iliotolewa na kundi la mawasiliano kuhusu Venezuela. Kundi hilo, linaloundea na mataifa ya Umoja wa Ulaya na Amerika Kusini, limetoa wito wa kuumaliza kwa amani mgogoro wa Venezuela, na kupendekeza kuwa njia bora y akufanyahivyo ni kuitisha uchaguzi.

"Mataifa ya Ulayana serikali ya Ujerumani wanamuunga mkono kikamilifu Guaido," Niels Annen, naibu waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani aliiambia DW. Annen alisema hatua zinahitajikakuchukuliwa ili kuhakikisha uchaguzi huru na wa haki unafanyika nchini Venezuela, na kuongeza: "Hili ni jambo bwana Maduro anapaswa kulikubali."

Kundi la mawasiliano lilitoa taarifa siku ya Alhamisi, likisema kuwa litatuma ujumbe wa kiufundi nchini Venezuela kuhakikisha uwasilishwaji wa msaada wa kiutu na kwamba litaunga mkono kura ya kitaifa.

"Hatukubaliani na maudhui ya waraka huo," Maduro alisema. "Tunakataa uhalisia wa kiitikadi na uelemeaji upande wa waraka wa kundi la mawasiliano."

Venezuela Juan Guaido trifft Studentenbewebung in Caracas
Juan Gauido akizungumza na wanafunzi wa chuo kikuu cha Central mjini Caracas -08.02.2019.Picha: picture-alliance/AA/M. Perez Del Carpio

Venezuela ambayo tayari imedhoofishwa kabisaa kutokana na sera ya kiuchumi za Maduro, ilitumbukia katika mgogoro wa kisiasa mwaka uliopita, alipopunguza pakubwa mamlaka ya bunge la taifa linalodhibitiwa na upinzani, na kuunda bunge sambamba ambalo lilitoa udhibiti zaidi kwa majimbo  ya nchi ambako ana umaarufu zaidi.

Januari 23, Gauido ambaye ni spika wa bunge la taifa, alitumia kipengele kisichoeleweka vizuri cha katiba ya Venezuela kujitangaza kuwa rais wa muda. Marekani, Canada na pia mataifa mengi ya Ulaya na Amerika Kusini, yamemtabua Guaido kama kiongozi wa muda na kuitisha uchaguzi mpya.

Guaido amekataa kuondoa uwezekano wa kuiruhusu Marekani kuingilia kati kumlaazimisha Maduro kuruhusu uingizwaji wa misaada ya kiutu na pia kuondoka madarakani.

Mwandishi: Iddi Ssessanga/DW

Mhariri: Zainab Aziz