1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VATICAN CITY :Papa awashukuru Wayahudi na Waislamu

6 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFZ5

Papa John Paul wa Pili aliekuwa akisubiriwa kwa hamu amejitokeza kwenye dirisha la ghorofa ya 10 kwenye hospitali aliyolazwa mjini Rome na kuupungia umati wa watu 300 uliokuwa chini ukiimba nyimbo za dini na kutowa ishara ya msalaba.

Papa mwenye umri wa miaka 84 ambaye amekuwa akipata nafuu kutokana na operesheni ya koo alionekana kukonda lakini katika hali nzuri na hakujaribu kuuhutubia umma huo wakati wa kujitokeza kwake kwa muda mfupi.

Muda mfupi kabla katika ujumbe uliosomwa na msaidizi wake kwa maelfu ya waamuni wa Kikristo na watalii katika uwanja wa St.Peter Papa aliwashukuru hususan Wayahudi na Waislamu kwa kumuombea apate nafuu.