1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uturuki yaonya kuendeleza mashambulizi Syria

Admin.WagnerD29 Agosti 2016

Uturuki imeonya kufanya mashamabulizi zaidi dhidi ya wanamgambo wa Kikurdi walioko Syria iwapo watashindwa kurudi nyuma huku Marekani ikilani mashambulio yao mwishoni mwa wiki kama jambo lisilokubalika.

https://p.dw.com/p/1Jrpa
Picha: picture-alliance/dpa/S. Suna

Uturuki imeendelea na operesheni zake kuu mbili ndani ya Syria dhidi ya wanajihadi wa kundi la Dola la Kiislamu na wapiganaji wa Kikurdi wa kundi la YPG kwa kushambulia kwa mizinga maeno yao kadhaa.

Uturuki imesema imeuwa magaidi 25 wa Kikurdi katika maeneo yanayokaliwa na kikosi cha YPG nchini Syria ambacho Uturiki inakiona kuwa ni cha kigaidi hapo jana, siku moja baada ya mwanajeshi wa Uturuki kuuawa na shambulio la roketi lililorushwa na wanamgambo hao.

Operesheni hiyo ya Uturuki inakusudia kuwarudisha nyuma wapiganaji wa kikosi hicho kupitia Mto Euphrates ili kuwazuwiya kuliunganisha eneo la mashariki mwa mto huo ambalo tayari liko kwenye udhibiti wao na lile lanaliloshikiliwa na Wakurdi lilioko magharibi.

Kundi la YPG latakiwa kurudi nyuma

Makamo wa Rais wa Marekani Joe Biden alipokuwa ziarani nchini Uturuki wiki iliopita amesema Marekani imekitaka kikosi hicho cha YPG kirudi nyuma kuvuka Mto Euphrates venginevyo litaachwa kuungwa mkono na Marekani.Uturuki imesema haikuona ushahidi wa kundi hilo likiitikikia wito huo wa Marekani.

Wapiganaji Wakikurdi wa kikosi cha YPG nchini Syria.
Wapiganaji Wakikurdi wa kikosi cha YPG nchini Syria.Picha: Getty Images/AFP/D. Souleiman

Akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Ankara waziri wa mambo ya nje wa Uuruki Mevlut Cavusoglu amesema lengo la operesheni yao hiyo ni kulitokomeza kundi la Dola la Kiislamu na amewashutumu wapiganaji wa Kikurdi wa YPG kwa kuhusika na mauaji ya kuokomeza kizazi cha jamii ya wachache.

Mevlut amesema " Lengo la operesheni hii ni kulisafisha eneo hili kwa kulindowa kundi la kigaidi la Daesh.Haiwezekani kulishinda kundi hili kwa mashambulizi ya anga pekee na kwamba operesheni za ardhini zinahitajika kulitokomeza kundi hilo kutoka Syria na Iraq."

Waziri huyo wa mambo ya nje wa Uturuki amekaririwa pia akisema katika maeneo ambayo wapiganaji wa Kikurdi wa YPG wameingia kila mtu aliyekuweko huko wakiwemo Wakurdi wenyewe wanaona jinsi wanavyofanya mauaji ya kutokemeza vizazi vya jamii ya wachache.

Amesema mchanganyiko wa jamii za wachache katika eneo karibu na mji wa Manbij magharibi mwa Mto Euphrates lilil otekwa na YPG kutoka kundi la Dola la Kiialamu kwa kiasi kikubwa walikuwa Waarabu.

Amesema wale waliokuwa wakiishi hapo wanapaswa kurudi badala ya kuwaweka wahamiaji wapya wa Kikurdi.

Wasi wasi wa Marekani

Wakati huo huo waziri wa Uturuki anayeshughulikia masuala ya Umoja wa Ulaya amesema hakuna mtu mwenye haki ya kuichagulia Uuruki kundi la kigaidi la kupambana nalo wakati nchi hiyo mwanachama wa Jumuia ya Kujihami ya NATO ikishutumiwa kwa kujiingiza kwake nchini Syria.

Makamo wa Rais wa Marekani Joe Biden na Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki wakati makamo huyo wa rais alipoitembelea nchi hiyo.
Makamo wa Rais wa Marekani Joe Biden na Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki wakati makamo huyo wa rais alipoitembelea nchi hiyo.Picha: picture alliance/AP Images/K. Ozer

Omer Celik amesema hakuna mtu mwenye haki ya kuwaambia kundi gani la kigaidi wapambane nalo na lipi walipuuze.

Marekani imekuwa ikielezea wasi wasi wake kwamba mapambano hayo ya Uturuki yamebadili mweleko badala ya kulilenga zaidi kundi la Dola la Kiislamu.

Marekani inawaunga mkono wapiganaji wa Kikurdi wa YPG katika mapambano dhidi ya kundi la Dola la Kiislamu.

Mwandishi ; Mohamed Dahman/Reuters/AFP

Mhariri:Iddi Ssessanga