Uturuki tayari kupatanisha kati ya Israel na Syria:
25 Januari 2004Matangazo
DAVOS: Uturuki imesema itayari kupatanisha katika mgogoro kati ya Israel na Syria. Nchi hizo mbili zimekwisha toa ishara za kuukubali upatanishi wa Uturuki, alisema Waziri Mkuu wa Uturuki Recep Tayyep Erdogan katika Mkutano wa Kimataifa wa Kiuchumi mjini Davos, Uswissi. Waziri wake wa Mambo ya Nje Abdullah Gül karibuni ataanzisha harakati hizo za kupatanisha, alisema Waziri Mkuu Erdogan. Kiini cha mgogoro kati ya Israel na Syria ni ile milima ya Goland iliyo milki ya Syria ambayo Israel iliiteka katika vita vya mwaka 1967. Israel inaendelea kuikatalia Syria dai lake la kurejeshewa milima hiyo kwenye mpaka wa nchi mbili.