1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Utawala wa Koroma washutumiwa kufuja pesa

3 Aprili 2019

Ripoti ya ukaguzi wa hesabu za serikali iliyotolewa na wizara ya fedha nchini Sierra Leone imeutuhumu utawala wa rais wa zamani Ernest Bai Koroma kwa ufujaji wa zaidi ya dola bilioni moja.

https://p.dw.com/p/3GAb9
Belgien Ebola Konferenz in Brüssel
Picha: T. Charlier/AFP/Getty Images

Waziri wa fedha Jacob Jusu Saffa ameahidi kuzirudisha fedha zote zilizoibiwa ili zisaidie katika mahitaji ya msingi ya wananchi wa taifa hilo.

Saffa ametoa ahadi hiyo baada ya ripoti ya ukaguzi wa matumizi ya fedha za serikali kuonesha kulikuwa na pengo kubwa katika fedha za umma wakati wa kipindi cha muongo mmoja wa utawala wa Koroma kuanzia mwezi Septemba hadi Aprili mwaka 2018.

Ripoti hiyo imeonesha kuna ukiukwaji mkubwa uliofanyika katika mchakato wa kutowa kandarasi kwenye miradi ya sekta ya nishati, barabara na malipo ya uzeeni pamoja na huduma za mawasiliano.