1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Utata wa Uingereza katika Brexit

30 Machi 2017

Uingereza inaonekana kuipuuza hatma ya mahusiano ya kiusalama na Umoja wa Ulaya katika kipindi hiki ambacho taifa hilo na umoja huo kwa mawa ya kwanza kabisa zikiweka wazi kabisa tofauti zao.

https://p.dw.com/p/2aMYX
Belgium EU Brexit
Picha: picture alliance/AP Photo/T.Monasse

Ufaransa na Ujerumani vilevile wameibuka na jitihada ya pamoja dhidi ya wito wa Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May wa kutaka mazungumzo ya kujiondoa na wakati huo huo mahusiano mapya, na hivyo kuibua kikiwazo kikubwa kabla hata mazungumzo yenyewe kuanza. Lakini ikiwa imepita siku moja baada ya May kutoa taarifa rasimi ya lengo la Uingereza kujiondoa, yeye huyo huyo alitoa onyo kwamba kushindwa kukifikia makubaliano ya kibiashara kutadhoofisha vita didi ya ugaidi.

Waziri mwenye dhamana na mchakato huo wa kujiondoa-Brexit David Davis alikiambia kituo cha radio cha BBC baada ya onyo hilo akiwa Brussels kwamba si kitishio na kwamba linaonekana kuingizwa kwa lengo la kuleta unafuu katika mazungumzo.  Amesema ni ukweli ulio wazi kabisa pasipo kuwa na mpango wa  pamoja na Ulaya, Uingereza haitaendelea kuwa taifa mwanachama wa shirika la kukabiliana na uhalifu la Ulaya Europol au kushiriki katia mfumo wa pamoja wa waranti katika umoja huo.

Uingereza ina taarifa muhimu kwa Ulaya

Großbritannien Brexit Theresa May Downing Street
Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa MayPicha: Reuters/H. Mckay

Waziri wa Mambo ya Ndani Amber Rudd, amesema kama wakitoka katika Europl, wataondoka na taarifa zao. Na mpatanishi mkuu katika mchakato wa Brexit, katika bunge la Umoja wa Ulaya Guy Verhofstadt alitilia alijibu mapigo kwa kusema suala la usalama wa wananchi limewekwa mbali na kwamba kama limechuliwa mateka katika majadiliano.

Mnyukano huo umeibuka wakati baadhi ya viongozi wa juu wa ulaya wakianzisha madala mkali katika kipindi hiki umoja huo ukijikongoja kutokana na pigo la kuondokewa moja kati ya wanachama wake wakubwa, kuwa wa kwanza kujiiondoa katika umoja huo tangu kuanzishwa kwake miaka 60 iliyopita.

Alhamis hii, Rais Francois Holland wa Ufaransa alifuata nyendo za Kansela Angela Merkel wa Ujerumani kwa kubeza pendekezo la muundo wa kujiondoa la May. kwa kusema makubaliano ya kujitoa yanapaswa kuwa ya kwanza kuanza kabla ya vyote. Hollande amesema lazima waanze mjadala wa namna ya kujiondoa, na hasa kwa kuzingatia matwaka ya wananchi na ahadi zilizo katika majukumu yaliywekwa na Uingerea kama taifa.

Miongoni mwa ajenda kubwa muhimu kwa viongozi hayo wa Ulaya ni pamoja na hatma ya raia milioni tatu wa Umoja wa Ulaya wanaoishi Uingereza na idadi nyingine ya Waingereza milioni moja ambao nao wanaishi katika mataifa yalio katika Umoja huo. Viongozi wa mataifa 27 ya umoja huo yanatarajiwa kufanya mkutano mkuu maalumu wa kilele Aprili 29 wenye lengo la kufanya mapitioa ya mipango iliyoainishwa. Raia wa Uingerza mwaka uliopita alipiga kura kwa asilimia 52 kwa 48 kujiondoa kwa taifa lao baada ya kufanyika kwa kampeni kali.

Mwandishi: Sudi Mnette AFP
Mhariri: Yusuf Saumu