1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Utaratibu wa kuidhinisha katiba ya Ulaya utaendelezwa licha ya "la" ya Uholanzi na Ufaransa

2 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF7b

Brussels

Viongozi wa taifa na serikali wa Umoja wa Ulaya wameonyesha wamevunjwa moyo na kura ya „La“ ya wadachi dhidi ya katiba ya umoja huo.Kansela Gerhard Schröder ametahadharisha juu ya hatari ya kuzuka mzozo barani Ulaya.Hata rais wa Ufaransa Jacques Chirac na waziri wa mambo ya nchi za nje wa Uengereza Jack Straw wameelezea masikito yao.Mwenyekiti wa zamu wa Umoja wa Ulaya waziri mkuu wa Luxembourg,Jean Claude Juncker,mwenyekiti wa kamisheni kuu Jose Manuel Barroso na spika wa bunge la Ulaya Joseph Borell wamesema,utaratibu wa kuidhinisha katiba utaendelea licha ya katiba hiyo kupingwa na wafaransa na wadachi .Bwana Jean Claude Juncker amesisitiza „na nchi nyengine zilizosalia zina haki pia ya kutoa maoni yao juu ya katiba ya umoja wa Ulaya.Waziri mkuu wa Danemark Anders Fogh RASMUSSEN ameahidi kura ya maoni itaitishwa nchini mwake kama ilivyopangwa mwezi september ujao.Na huko pia utafiti wa maoni ya watu unaashiria kura ya La itashinda.