1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Utafiti: Saratani za chini ya miaka 50 zaongezeka

6 Septemba 2023

Utafiti wa kimataifa uliochapishwa hii leo umeonyesha visa vya saratani vikiongezeka kwa watu wa chini ya miaka 50, kutoka milioni 1.82 hadi milioni 3.26 katika kipindi cha miongo mitatu.

https://p.dw.com/p/4W1UD
Seli za Saratani
Picha ya seli za saratani katika 3DPicha: ersin arslan/Zoonar/picture alliance

Utafiti wa kimataifa uliochapishwa hii leo umeonyesha visa vya saratani vikiongezeka kwa watu wa chini ya miaka 50, kutoka milioni 1.82 hadi milioni 3.26 katika kipindi cha miongo mitatu. Ongezeko hilo ni sawa na asilimia 79.1.

Watafiti wametumia takwimu za tangu mwaka 2019 za uchunguzi uliofanywa na taasisi ya Global Burden of Disease iliyoainisha viwango vya aina 29 za saratani katika mataifa 204.

Utafiti kuhusu dawa za kutibu saratani: Tafiti za saratani: Je dawa zilizopo zinatibu?

Watafiti hao wanasema, vichocheo vikubwa vya saratani kuwa ni ulaji mbaya na matumizi ya sigara na pombe kwa rika hilo, lakini wakikiri bado hakuna sababu ya wazi juu ya mwenendo wa ongezeko hilo, ingawa ongezeko la idadi ya watu pia linachangia.

Utafiti huo uliochapishwa katika jarida la BMJ Oncology umefanywa kwa ushirikiano na chuo vyuo vikuu vya Edinburgh cha Scotland na Zhejiang cha China, pamoja na Marekani na Sweden, umezitaja sababu nyingine zinazoweza kuchangia kuwa ni uzito mkubwa na kutofanya mazoezi.