1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Usitishaji mapigano waendelea kuheshimiwa, Congo

29 Novemba 2022

Hatua ya usitishaji mapigano kati ya wanajeshi wa serikali na waasi wa kundi la M23 yanaonesha yanayendelea kuheshimiwa,kwa siku ya tatu hapo jana Jumatatu,katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

https://p.dw.com/p/4KER4
Kongo | Demokratische Republik Kongo DRC Soldaten
Picha: Guerchom Ndeb/AFP/Getty Images

Kwa mujibu wa wakaazi hatua hiyo inashuhudiwa licha ya kuwepo makabiliano kati ya makundi ya waasi yanayokinzana. 

Makubaliano hayo yalifikiwa Ijumaa usiku ambapo kundi la M23 lilitakiwa kuondoa wapiganaji wake katika maeneo mengi wanayoyakamata huko mashariki mwa Kongo,la sivyo wakabiliwe na nguvu za kijeshi za kikosi cha Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Wakaazi wa maeneo hayo waliripoti jana kwamba kuna hali ya utulivu ingawa shirika la habari la AFP limesema halikuweza kuthibitisha yaliyoelezwa na wakaazi hao.

Kundi la M23 linadhibiti eneo kubwa la mji wa Rutshuru ulioko kaskazini mwa Goma,mji ambayo unakaliwa na watu milioni moja.
 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW