1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Usain Bolt kuanza kucheza soka Australia

Sekione Kitojo
29 Agosti 2018

Timu ya mkimbiaji maarufu wa zamani duniani Usain Bolt Central Coast Mariners ambapo  kwa mara ya kwanza ananza kuichezea  timu hiyo kwa mara ya kwanza, itakutana dhidi ya timu ya wafanyakazi wa ofisini, na wa viwandani.

https://p.dw.com/p/33wVN
Australien Usain Bolt beim Training der Central Coast Mariners
Picha: picture-alliance/dpa/AAP/D. Himbrechts

Timu  hiyo  ya  wachezaji  ambao  si  wa  kulipwa  haina nia  kabisa  na  kumpa bingwa  huyo  wa  mbio katika michezo  ya  olimpiki nafasi  ya  kutamba  tena, amesema nahodha  wa  timu  hiyo Matt Page.

Mjamaica  huyo  anamatumaini  ya  kupata  mkataba  wa kulipwa katika  ligi  ya  Australia na  atakuwa  katika  hatua za  kujaribiwa  siku  ya  Ijumaa  wakati  timu  yake  Mariners itakapocheza  na  kikosi  cha  wachezaji  ambao  si  wa kulipwa  katika  mji  wa  Gosford , kaskazini  mwa  Sydney.

Australien Usain Bolt beim Training der Central Coast Mariners
Usain Bolt akifanya mazowezi na timu yake ya MarinersPicha: Getty Images/T. Feder

Mchezo  huo  wa  kabla  ya  kuanza  kwa  msimu utaoneshwa  moja  kwa  moja  katika  televisheni  na  kituo cha  televisheni  katika  mji  huo  na  unaweza  kuwavuta zaidi  ya  mashabiki 12,000  uwanjani  katika  uwanja  wa nyumbani  wa  Mariners, ambako  watatarajia  mchezo  wa kasi, na  huenda  kujitokeza  kwa  nyota  huyo wa  riadha kuwa  kivutio  kikubwa.

Bolt  hata  hivyo  ana  weza  kutarajia  kukumbana  na wapinzani ambao  watakuwa  na  nia  ya  kujionesha kwa mashabiki  watakaokuwa  wakiangalia  mchezo  huo.

China - Olympische Sommerspiele 2008 in Peking: Usain Bolt gewinnt Gold mit Weltrekordzeit
Usain Bolt wakati akiwa mkimbiaji wa mbio za mita 100Picha: picture-alliance/L. Perenyi

Bingwa  mara  nane  wa  medali  ya  dhahabu katika michezo  ya  Olimpiki  Bolt  alifanya  mazowezi  yake  ya mwanzo  na  timu  hiyo  ya  daraja  la  kwanza  nchini Australia  wiki  moja  iliyopita na  kusema  anatarajia atajisikia  na  wasi  wasi  kidogo  katika  mchezo  huo  wa majaribio. Amekiri  kwamba  bado  hayuko  fit  na  bado anahangaika  na  hali  ya  kusimama  na  kuanza tena katika mchezo  wa  kandanda.

Mwandishi: Sekione  Kitojo / rtre

Mhariri: Idd Ssessanga