1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Von der Leyen atowa hotuba katika bunge la Umoja wa Ulaya

13 Septemba 2023

Rais wa Halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula Von der leyen ametowa hotuba yake ya kila mwaka kuhusu sera zake katika bunge la Umoja huo, akisisitiza zaidi juu ya mafanikio yake.

https://p.dw.com/p/4WHUN
EU Parlament Kommissionspräsidentin Ursula von der Leyen Rede
Picha: Jean-Francois Badias/AP Photo/picture alliance

Von der Leyen amejiepusha kuzungumzia kuhusu ikiwa anataka kuwania muhula wa pili kwenye nafasi hiyo. 

Miongoni mwa aliyoyagusia kwenye hotuba hiyo aliyoitowa  mbele ya bunge la Umoja wa Ulaya,mjini Strassburg,ni suala la Ukraine akisema mustakabali wa nchi hiyo uko mikononi mwa Umoja wa Ulaya.

Amesema Ukraine imechukuwa hatua kubwa katika juhudi zake za kutaka kuwa mwanachama wa Jumuiya hiyo na kazi sio rahisi. Ameahidi kwamba  jumuiya hiyo itaendelea kuwapa ulinzi raia wa nchi hiyo waliokimbia vita vya Urusi.

Kwenye hotuba yake hiyo inayotowa mwelekeo wa sera zake,pia ameapa kuitetea sekta ya viwanda ya Umoja wa Ulaya dhidi ya viwango vya chini vya bei ya magari ya umeme yanayotengenezwa na  China.