1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Urusi yashambulia vituo vya nishati magharibi mwa Ukraine

26 Agosti 2024

Urusi imevishambulia vituo vya nishati vilivyoko katika mji wa Lviv magharibi mwa Ukraine, hii ikiwa ni kulingana na gavana wa eneo hilo hii leo, wakati maeneo kadhaa kote nchini humo yakiripoti mashambulizi ya mabomu.

https://p.dw.com/p/4jvDq
Ukraine Mkoa wa Odessa | Moto kutokana na shambulio la Urusi
Moto uliozuka kutokana na shambulizi la Urusi kwenye mkoa wa Odesa.Picha: Press Service of the State Emergency Service of Ukraine in Odesa region/Handout/REUTERS

Gavana Maksym Kozytskyi amesema kupitia mitandao ya kijamii kwamba mashambulizi hayo yamesababisha kukatika kwa umeme kwenye jiji la Lviv na eneo hilo zima.

Taarifa zimesema vikosi vya Urusi vilifanya mashambulizi makubwa ya droni dhidi ya Ukraine tangu jana usiku na kuendelea hadi hii leo na ambayo yanachukuliwa kuwa makubwa zaidi katika kipindi cha wiki kadhaa.

Huku hayo yakiendelea, afisa wa ngazi za juu wa ofisi ya rais wa Ukraine amewaomba washirika wake kuiruhusu kuishambulizi Urusi kwa makombora ya masafa marefu iliyopewa na magharibi, kufuatia mashambulizi haya ya leo.