1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Urusi yashambulia kwa droni Kyiv na mji wa bandari Odesa

6 Oktoba 2024

Urusi ilifyatua ndege zisizo na rubani usiku kucha katika na kote Ukraine na kulenga mji mkuu Kyiv pamoja na miundombinu katika bandari ya Bahari Nyeusi ya Odesa. Hayo yamesemwa na maafisa wa Ukraine.

https://p.dw.com/p/4lSQv
Ukraine | Odessa
Wazima moto wanajaribu kuzima moto ulioharibu miundombinu ya raia iliyoharibiwa huko Odesa.Picha: State Emergency Service of Ukraine/Anadolu/picture alliance

Kwa mujibu wa Huduma ya Dharura ya Ukraine mtu mmoja amejeruhiwa huku maghala na malori ya mizigo yakiharibiwa katika msururu wa mashambulizi ambayo yaliweka sehemu kubwa ya nchi hiyo kuwa katika tahadhari ya uvamizi wa anga kwa saa kadhaa.

Soma pia: Urusi na Ukraine zaendelea kushambuliana

Jeshi la anga limedai kudungua droni 56 kati ya 87 zilizovurumishwa na Urusi kuelekea maeneo mbalimbali ya nchi.

Hata hivyo Urusi imekanusha kuwalenga raia lakini mara kwa mara hurusha makombora, ndege zisizo na rubani na mabomu katika maeneo ya makaazi mbali na kwenye mstari wa mbele wa vita.