1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yaishambulia mikoa tisa ya Ukraine kwa droni

3 Agosti 2024

Urusi imefanya shambulio la droni nchini Ukraine usiku wa kuamkia leo na kuharibu miundombinu muhimu katika mji wa Vinnytsia uliopo katikati mwa nchi hiyo. Hayo yamesemwa na Afisa wa eneo hilo.

https://p.dw.com/p/4j4la
Ukraine
Wafanyakazi wa uokozi katika mji wa Vinnytsia nchini Ukraine wakipamban kuuzima moto uliosababishwa na shambgulizi la Urusi Picha: rainian Emergency Service via AP Photo/picture alliance

Urusi imefanya shambulio la droni nchini Ukraine usiku wa kuamkia leo na kuharibu miundombinu muhimu katika mji wa Vinnytsia  uliopo katikati mwa nchi hiyo. Hayo yamesemwa na Afisa wa eneo hilo.

Jeshi la anga la Ukraine limesema limezidungua droni 24 kati ya 29 aina ya Shahed zilizorushwa na Urusi katika shambulio hilo la usiku katika mikoa zaidi ya tisa. Gavana wa mkoa wa Mykolaiv,Vitaliy Kim, amesema licha ya droni hizo kudunguliwa lakini bado zilisababisha moto katika majengo ingawa mpaka sasa hakuna majeruhi walioripotiwa.

Mapema wiki hii, Ukraine ilisema iliyazuia moja ya mashambulizi makubwa zaidi ya droni za Urusi tangu Februari 2022 ambapo ulinzi wake wa anga ulizidungua droni 89 zilizolenga kuharibu mifumo yake ya ulinzi.