1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yaionya Japan kuipa Ukraine mfumo wa ulinzi wa anga

27 Desemba 2023

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Urusi Maria Zakharova amesema hatua ya Japan kutoa mfumo wa ulinzi wa anga aina ya Patriot kwa Ukraine itakuwa na majibu makali.

https://p.dw.com/p/4adA2
Urusi | Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Urusi Maria Zakharova
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Urusi Maria ZakharovaPicha: Petrov Sergey/Russian Look/IMAGO

Amesema hilo linatishia kuharibu uhusiano wa Japan na Urusi. Wiki iliyopita Japan ilisema inajiandaa kupeleka mifumo hiyo ya ulinzi wa anga nchini Marekani baada yakupitia kanuni za usafirishaji wa silaha zake.

Licha ya kanuni za taifa hilo la Asia kuizuwia nchi hiyo kusafirisha silaha kwa nchi zilizo vitani, inaweza kuifaidisha Ukraine sio moja kwa moja, kwa kuipa Marekani silaha ili Marekani izisafirishe mjini Kiev.

Soma pia:Ukraine yasema imedungua droni za Urusi

Mahusiano kati ya Moscow na Tokyo ambayo tayari yanayumba yamezidi kuingia doa tangu Urusi ilipotuma maelfu ya wanajeshi wake  nchini Ukraine Februari mwaka 2022, baada ya hapo Japan ilijiunga na washirika wa Magharibi kuiwekea vikwazo Urusi kufuatia hatua yake hiyo.