1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Urusi yadai kusonga mbele kilometa 1,000 ndani ya Ukraine

11 Septemba 2024

Urusi imesema vikosi vyake vimesonga mbele kwa kilometa 1,000 za mraba mashariki mwa Ukraine kati ya Agosti na Septemba licha ya shambulizi la kuvuka mpaka lililofanywa na wanajeshi wa Ukraine ndani ya ardhi ya Urusi.

https://p.dw.com/p/4kU3D
Uwanja wa mapambano huko Donbas mashariki mwa Ukraine
Uwanja wa mapambano huko Donbas mashariki mwa Ukraine. Picha: Svet Jacqueline/Zumapress/picture alliance

Katibu Mkuu wa Baraza la Usalama la Urusi Sergei Shoigu amesema lengo la shambulizi la Ukraine la Agosti 6 ndani ya jimbo la Urusi la Kursk lilikuwa na dhamira ya kuongeza usemi wa nchi hiyo kwenye meza ya mazungumzo na kuhamisha nguvu ya jeshi la Moscow kutoka jimbo la mashariki mwa Ukraine la Donbas.

Amesema hata hivyo dhamira hiyo haijafanikiwa na sasa vikosi vya Urusi vimesonga mbele ndani ya ardhi ya Ukraine na kulikamata eneo la ukubwa wa kilometa 1,000 za mraba.

Hapo jana wizara ya ulinzi ya Urusi ilitangaza kuvikamata vijiji vinne vya Ukraine kwenye eneo hilo, ingawa Ukraine imepinga baadhi ya maelezo yaliyotolewa na Moscow.