1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Urusi na Ukraine zashambuliana vikali usiku kucha

31 Agosti 2024

Watu watano wameuawa na wengine 37 wamejeruhiwa katika eneo la mpakani la Urusi la Belgorod kufuatia mashambulizi ya Ukraine.

https://p.dw.com/p/4k7mW
Askari wa Ukraine akishuhudia kufyetuliwa kwa kombora kuelekea ardhi ya Urusi
Askari wa Ukraine akishuhudia kufyetuliwa kwa kombora kuelekea ardhi ya UrusiPicha: Libkos/AP/dpa/picture alliance

Gavana wa eneo hilo Vyacheslav Gladkov ameandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Telegram kwamba waliuawa ni  mwanamke mmoja na wanaume wanne baada ya Ukraine kuvurumisha idadi kubwa ya makombora.

Urusi nayo ilishambulia kwa mabomu mji wa kaskazini mashariki mwa Ukraine wa Kharkiv na kulilenga jengo moja la makazi na uwanja wa michezo, na kusababisha vifo vya watu sita huku wengine zaidi ya 55 wakijeruhiwa.

Soma pia:Urusi na Ukraine zakabiliana vikali 

Kiev imewatolea wito washirika wake kuipatia mifumo zaidi ya ulinzi wa anga, huku Urusi ikiwaondoa mamluki wake nchini Burkina Faso ili kusaidia kukabiliana na uvamizi wa Ukraine huko Kursk.