1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi na Ukraine wabadilishana wafungwa wa vita

24 Agosti 2024

Urusi na Ukraine wamebadilishana wafungwa wa vita 115 kutoka kila upande, katika tukio lililosimamiwa na Umoja wa Falme za kiarabu.

https://p.dw.com/p/4jsxE
Ukraine | Urusi
Urusi na Ukraine wabadilishana wafungwa wa vita Picha: Ukraine's President Volodymyr Zelenskiy/Telegram/Handout/REUTERS

Huu ni ubadilishanaji wa kwanza wa aina hii kufanyika tangu Ukraine ilipoanzisha shambulizi la kushtukiza katika eneo la Urusi la Kursk mnamo Agosti 6, shambulizi linalosemekana kuwa kubwa kabisa kufanywa nchini Urusi na taifa la kigeni tangu kumalizika kwa vita vya pili vya dunia. 

Wanajeshi wote wa Urusi walioachiwa,  sasa wapo Belarus watakakopokea matibabu kabla ya kurejeshwa nchini mwao. 

Putin aishtumu Ukraine kujaribu kukishambulia kinu cha nyuklia

Wakati huo huo rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy alichapisha picha ya wafungwa hao wa vita wa nchi yake wakiwa wamejifunika kwa bendera ya taifa hilo ya rangi ya buluu na njano. Zelesnky amesema walioachiwa walikuwa walinzi wa mpakani, wa taifa, wa jeshi la majini na wanajeshi wa ardhini.

Umoja wa Falme za kiarabu UAE imethibitisha jukumu lake la kushiriki juhudi za kuachiwa kwa wafungwa hao ikisema kupitia wizara ya mambo ya nje kwamba idadi ya wafungwa walioachiliwa tangu ichukue jukumu hilo imefikia 1,788.