1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaZimbabwe

Upinzani Zimbabwe waitisha maandamano kupinga uchaguzi

Sylvia Mwehozi
1 Septemba 2023

Chama kikuu cha upinzani nchini Zimbabwe kimeitisha maandamano ya kitaifa siku ya Ijumaa na kutoa mwito wa kurudiwa kwa uchaguzi ambao kimesema uligubikwa na udanganyifu uliomrejesha mamlakani rais Emmerson Mnangagwa.

https://p.dw.com/p/4Vq9E
Simbabwe Afrika Veranstaltung Opposition
Picha: KB MPOFU/REUTERS

Mwito huo kutoka kwa chama cha Citizens Coalition for Change (CCC) umetolewa siku moja baada ya Mnangagwa kusema uchaguzi ulikuwa halali, huku akionya yoyote atakayesababisha ghasia atachukuliwa hatua kali.

Maandamano hayo yatafanyika katika majimbo 10 ya Zimbabwe , huku chama hicho kikiwaomba wanaharakati kuanzisha kampeni za mitandaoni na kusambaza ushahidi wa udanganyifu uliofanyikwa kwenye uchaguzi huo. CCC kina siku saba za kuwasilisha madai ya kupinga matokeo hayo ya uchaguzi mahakamani, tangu tume ilipotangaza rasmi.

Tume ya taifa ya uchaguzi ya Zimbabwe ilimtangaza Mnangagwa kushinda uchaguzi kwa asilimia karibu 53 na mpinzani wake Nelson Chamisa wa CCC akipata asilimia 44.