1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Upinzani Venezuela waitisha maandamano ya dunia Agosti 17

12 Agosti 2024

Upinzani nchini Venezuela umeitisha maandamano dunia nzima Agosti 17 kuonyesha uungaji mkono kwa madai yake ya ushindi katika uchaguzi wa mwezi uliyopita dhidi ya Rais Nicolas Maduro.

https://p.dw.com/p/4jMZp
Venezuela I Uchaguzi -  Edmundo Gonzalez
Kiongozi wa upinzani wa Venezuela Maria Corina Machado na mgombea urais Edmundo Gonzalez waakti wa kampeni.Picha: Alfredo Lasry R/Getty Images

Upinzani nchini Venezuela umeitisha maandamano dunia nzima Agosti 17 kuonyesha uungaji mkono kwa madai yake ya ushindi katika uchaguzi wa mwezi uliyopita dhidi ya Rais Nicolas Maduro, ambaye alitangazwa mshindi.

Katika ujumbe wa vidio iliyochapishwa kwenye mitandao ya kijamii, kiongozi wa upinzani Maria Corina Machado, alisema wataingia mitaani Jumamosi ijayo nchini Venezuela na kote ulimwengunu na wapige kelele pamoja ili ulimwengu uuge mkono ushindi wao na kutambua ukweli na mamlaka ya wananchi.

Soma zaidi: Wapinzani Venezuela wachunguzwa kwa makosa ya jinai

Mgombea wa upinzani Edmundo Gonzalez Urrutia, ambaye alichukuwa nafasi ya Machado baada ya kuzuwiwa kugombea, amesema walishinda, na kuwataka watu kujitokeza kwa wingi Jumamosi.

Viongozi hao wawili wamekuwa mafichoni kwa zaidi ya wiki sasa, huku Machado akisema anahofia maisha yake, baada ya wanachama kadhaa wa upinzani kuripotiwa kukamatwa.