1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Upinzani: EU usiutambue uchaguzi wa Belarus

19 Agosti 2020

Kiongozi wa upinzani nchini Belarus Sviatlana Tsikhanouskaya leo ametoa wito kwa viongozi wa Umoja wa Ulaya kutoutambua uchaguzi wa rais uliompa ushindi kiongozi wa muda mrefu  Alexander Lukashenko

https://p.dw.com/p/3hAzz
Belarus Präsidentschaftswahl Oppositionskandidatin Swetlana Tichanowskaja
Picha: picture alliance/AP Photo

Kiongozi wa upinzani nchini Belarus Sviatlana Tsikhanouskaya leo ametoa wito kwa viongozi wa Umoja wa Ulaya kutoutambua uchaguzi wa rais uliompa ushindi kiongozi wa muda mrefu  Alexander Lukashenko na kuzusha maandamano makubwa ya kupinga utawala wake.

Katika ujumbe wa video aliotoa kuelekea mkutano wa dharura uliotishwa leo na Umoja wa Ulaya kujadili hali nchini Belarus, Tsikhanouskaya amewataka viognozi wa kanda hiyo kuunga mkono vuguvugu la mageuzi kwenye taifa hilo la uliokuwa muungano wa kisovieti.

Kizungumkuti cha maridhiano ya baraza la uratibu wa uongozi wa Belarus

Weißrussland Protest-Kundgebung auf dem Platz der Unabhängigkeit in Minsk
Umati wa waandamanaji mjini MinskPicha: DW/A. Boguslavskaya

Lukashenko ambaye amelitawala taifa hilo la watu milioni 9.5 tangu 1994 alitangazwa mshindi kwa asilimia 80 katika uchaguzi wa Agosti 9 ambao upande wa upinzani umesema uligubikwa na wizi wa kura. Mapema wiki hii Tsikhanouskaya alisema yupo tayari kushika kwa muda wadhfa wa kiongozi wa kitaifa ili kuweza kuratibu marejeo ya uchaguzi. Lakini pia washiriki wake walitangaza kile walichokiita baraza la uratibu kwa ajili ya kusaidia makabidhiano ya madaraka kwa amani.

Soma zaidi: Umoja wa Ulaya watarajiwa kuwawekea vikwazo maafisa wa Belarus

Hata hivyo Lukashenko amerejea kwa mara kadhaa kukataa takwa la kujiuzulu na kupinga pia wazo la kufanya mazungumzo na upinzani, na kusema uratibu wa baraza kuwa ni sawa na jaribio la kunyikulia madaraka.