Unyanyasaji wa kingono waongezeka mjini Goma, DRC
10 Mei 2023Matangazo
Kulingana na shirika hilo la MSF, kuanzia Aprili 17 hadi 30, limekuwa likiwasaidia waathirika wapya 48 kwa siku na hasa katika maeneo ambayo watu wamekimbia makazi yao katika mji mkuu huo wa jimbo lenye migogoro la Kivu Kaskazini. Shirika hilo MSF limeongeza kwa kusema takriban asilimia 60 ya visa hivyo vinahusisha wanawake ambao walivamiwa katika muda wa saa 72 zilizopita. Jason Rizz ambaye ni mratibu wa matukio ya dharura katika shirika MSF amesema kwa miezi kadhaa wamekuwa wakishughulikia idadi kubwa ya matukio ya unyanyasaji wa kijinsia lakini haijawahi kufikia kiwango cha juu kama ilivyo katika majuma ya hivi karibuni nchini humo.