1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani ya Kusini

UN: Zaidi ya watu 2,400 wamefariki Haiti

18 Agosti 2023

Zaidi ya watu 2,400 wameuwawa nchini Haiti tangu mwanzoni mwa mwaka 2023 kutokana na machafuko.

https://p.dw.com/p/4VJgs
Machafuko yanayofanywa na magenge ya uhalifu yamekuwa yakiwahangaisha raia wa Haiti hasa wa mji mkuu Port-au-Prince tangu mwanzo wa mwaka huu 2023.
Machafuko yanayofanywa na magenge ya uhalifu yamekuwa yakiwahangaisha raia wa Haiti hasa wa mji mkuu Port-au-Prince tangu mwanzo wa mwaka huu 2023.Picha: Odelyn Joseph/AP Photo/picture alliance

Machafuko hayo yanatokana na magenge ya uhalifu. Haya ni kwa mujibu wa Shirika la Haki la Umoja wa Mataifa.

Msemaji wa shirika hilo Ravina Shamdasani amesema leo kuwa, miongoni mwa hao waliouwawa ni watu 350 waliouwawa kwa kuchomwa na wakaazi na makundi ya kulinda usalama. Umoja wa Mataifa unasema pia kwamba watu 902 wamejeruhiwa kuanzia Januari mosi hadi Agosti 15. T

aarifa hii ya Umoja wa Mataifa inakuja baada ya kundi moja la kutetea haki za kibinadamu huko Haiti kusema kwamba watu 30 waliuwawa jana katika Mji Mkuu Port-au-Prince na dazeni nyengine ya watu kujeruhiwa.

Mtandao wa kitaifa wa kutetea haki za binadamu nchini Haiti umesema pia kuwa nyumba katika mtaa wa Carrefour zilichomwa moto katika mashambulizi hayo na maafisa wawili wa polisi wakauwawa pia.