1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN yawakumbuka watumishi wake waliouawa Gaza

13 Novemba 2023

Bendera zimepepea nusu mlingoti kwenye majengo ya Umoja wa Mataifa kote ulimwenguni, huku watumishi wakikaa kimya kwa dakika moja ili kuwakumbuka wenzao zaidi ya 100 waliouawa Gaza katika vita vya Israel na Hamas.

https://p.dw.com/p/4Yl1l
Bendera ya Umoja wa Mataifa ikipepea nusu mlingoti mjini Nairobi kwa heshima ya waliouwawa Gaza
Bendera ya Umoja wa Mataifa ikipepea nusu mlingoti mjini Nairobi kwa heshima ya waliouwawa Gaza Picha: Simon Maina/AFP/Getty Images

Bendera zenye rangi nyeupe na bluu za Umoja huo kwa mara ya kwanza zilishushwa hadi nusu mlingoni majira ya saa 3.30 katika ofisi zake za Bangkok, Tokyo na Beijing na baadae zilishushwa kwenye ofisi nyingine. 

Shirika la Umoja huo linalowashughulikia wakimbizi wa Palestina, UNRWA lilitangaza siku ya Ijumaa kwamba watumishi 101 wamekufa katika Ukanda wa Gaza tangu vita hivyo vilipoibuka mwezi mmoja uliopita.

Mkurugenzi mkuu wa ofisi za umoja huo mjini Geneva, Tatiana Valovaya amewaambia watumishi kwamba idadi hii ni kubwa kuwahi kushuhudiwa katika kipindi kifupi kwenye historia ya Umoja wa Mataifa.