UN yatiwa wasiwasi na ripoti za M23 kusonga mbele Bukavu
31 Januari 2025Matangazo
Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujjarric, amesema pia kuwa ujumbe wa amani wa Umoja wa Mataifa MONUSCO, umeripoti juu ya vikosi vya Rwanda kuvuka mpaka na kuelekea upande huo.
"Tunafadhaika sana na hali ya sasa katika Kivu Kusini, hasa, ambayo bado ni tete, na kuna ripoti za kuaminika kwamba M23 inasonga kwa kasi kuelekea mji wa Bukavu," alisema Stephane Dujarric, msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres.
Waasi wa M23 waliosema kuwa wanataka kupigania mji mkuu wa Kongo, Kinshasa, walitoa kauli hiyo masaa machache baada ya Rais wa Kongo kuita kwa kuhamasisha jeshi kubwa kupambana na uasi huo.