1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN yalaani shambulizi la Algeria

12 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CagD

BALI.Umoja wa Mataifa umelaani vikali shambulizi la mabomu mawili hapo jana katika mji mkuu wa Algeria Algiers ambapo zaidi ya watu 60 waliuawa wakiwemo wafanyakazi wa umoja huo.

Katika taarifa yake akiwa huko Bali Indonesia kwenye mkutano wa hali ya hewa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon ameliita shambulizi hilo kuwa ni la kigaidi ambalo limeharibu ofisi za mashirika ya umoja huo za UNDP na UNHCR.

Wizara ya mambo ya ndani ya Algeria inasema kuwa waliyouawa katika shambulizi hilo ni 26, lakini vyanzo vya habari kutoka hospitali vinasema kuwa waliyouawa ni 62.

Tawi la kundi la al Qaida liitwalo Islamic Maghreb limedai kuhusika na shambulizi hilo.