1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN: Watoto milioni 5 wa chini ya miaka 5 walifariki 2021

10 Januari 2023

Umoja wa Mataifa umesema takribani watoto milioni tano wanakadiriwa walikufa kabla ya kufikisha umri wa miaka mitano mwaka 2021. Takwimu zimechapishwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linalokadiria Vifo vya Watoto, UNIGME

https://p.dw.com/p/4LwdP
Symbolbild I Milch I Afrika
Picha: Michael Gottschalk/photothek/picture alliance

Takwimu zilizochapishwa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa linalokadiria Vifo vya Watoto, UNIGME zimebaini kwamba watoto milioni 2.1 na vijana wenye kati ya umri wa miaka 5 hadi 25 wamepoteza maisha katika kipindi kama hicho. Kipindi hicho kinalingana na mtoto au kijana anayekufa kila sekunde 4.4. Taarifa tofauti ya shirika hilo pia imegundua kwamba watoto milioni 1.9 walifia tumboni mwaka 2021. Ripoti hiyo imefafanua kuwa vifo vingi vingeweza kuepukika kama kungekuwepo huduma bora za afya. Shirika la UNIGME limeonya kwamba takribani watoto na vijana milioni 59 watakufa kabla ya kufika mwaka 2030, kama hatua za haraka hazitochukuliwa kuimarisha huduma za afya.