1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya kufungua mipaka yake kwa waliochanjwa

19 Mei 2021

Duru kutoka Umoja wa Ulaya zinaripoti kwamba nchi wanachama wa umoja huo zimekubaliana leo kufungua mipaka ya nchi zao kwa wasafiri ambao wamechomwa chanjo kamili dhidi ya virusi vya corona.

https://p.dw.com/p/3td7y
Chinas Impfstoff Sinopharm
Picha: ROBERT ATANASOVSKI/AFP/Getty Images

Katika mkutano mjini Brussels, wanadiplomasia wa nchi hizo wamekubaliana kuongeza kiwango cha maambukizi ambacho kwa nchi iliyofikia itatangazwa kutokuwa salama.

Hatua hii inatarajiwa kutoa nafasi ya watu kuingia katika nchi za Umoja wa Ulaya kutoka nchi zengine.

Tangu Machi mwaka jana 2020 usafiri usio kwa sababu za lazima katika nchi za Umoja wa Ulaya umepigwa marufuku isipokuwa katika nchi chache tu zinazodchukuliwa kuwa salama kutokana na idadi yake ndogo ya maambukizi.