1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa UIaya hautambui ushindi wa Maduro

5 Agosti 2024

Msemaji wa mwanadiplomasia mkuu wa Umoja wa Ulaya Josep Borell, Peter Stano, amesema kuwa Umoja huo hautatambua matokeo ya uchaguzi wa urais nchini Venezuela.

https://p.dw.com/p/4j8Bt
Venezuela Nicolas Maduro
Rais Nicolas Maduro wa Venezuela.Picha: Matias Delacroix/AP Photo/picture alliance

Kupitia taarifa yake, Stano ameeleza kuwa jaribio lolote la kuchelewesha uchapishaji wa matokeo ya kura litazidi kutia mashaka juu ya uaminifu wa matokeo yaliyochapishwa na tume ya uchaguzi.

Baada ya uchaguzi wa Julai 28, tume ya uchaguzi ya Venezuela ilimtangaza Rais Nicolas Maduro, ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 2013, kuwa mshindi.

Soma zaidi: Shinikizo kwa Nicolas Maduro lazidi kuongezeka

Hata hivyo, tume hiyo bado haijachapisha matokeo ya kura katika majimbo huku kukiwa na madai ya wizi wa kura. 

Upinzani unaishtumu serikali kwa 'kuyachakachua' matokeo ya uchaguzi huo na unadai kuwa mgombea wake, Edmundo Gonzalez, ndiye mshindi halali.

Upinzani umesema umekusanya matokeo yao katika zaidi ya asilimia 80 ya majimbo nchini humo ambayo yanaonesha kuwa Gonzalez amepata asilimia 67 ya kura huku Maduro akipata asilimia 30 tu.