1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UMOJA WA MATAIFA:Kofi Annan aondolewa lawama juu ya mpango wa chakula kwa mafuta nchini Iraq

8 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEdF

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Kofi Annan amearifu kwamba matokeo ya uchunguzi huru juu ya mpango wa umoja wa mataifa wa mafuta kwa chakula nchini Iraq umewatia aibu kubwa wote waliohusika.

Paul Volcker mwenyekiti wa zamani wa benki kuu ya Marekani ambaye ndiye mkuu wa jopo la uchunguzi huo amemlaumu Kofi Annan kama katibu mkuu wa Umoja wa mataifa kwa kushindwa kuyafuatilia masuala kadhaa ya uongozi.

Ripoti hiyo inasema kwamba wale wote waliosimamia mpango huo walipuuza ushahidi uliowazi juu ya rushwa na ufujaji.

Hata hivyo lakini Volcker amemuondolea lawama katibu mkuu Annan za kuwa na mwenendo mbaya wa mfumo wa Uongozi.

Ripoti hiyo pia imeonyesha kwamba Umoja wa Mataifa unahitaji mageuzi ya haraka.