UN yatoa tahadhari na kuonya kuhusu ukosefu wa chakula
19 Aprili 2023Matangazo
Katika mkutano na waandishi wa habari katika mji mkuu wa Senegal, Dakar hapo jana, maafisa wa umoja huo walisema nchi zinazoathirika zaidi ni Burkina Faso, Mali, Niger na Mauritania ambazo ziko katika ukanda wa Sahel.
Afisa lishe wa shirika la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Watoto, UNICEF, Ann Defraye amesema hali inatisha na kuongeza kuwa mwaka uliopita ukanda huo wa Sahel ulisajiri asilimia 31 ya watoto wenye utapiamlo.
Miongoni mwa sababu za tatizo hilo, kulingana na maafisa hao ni athari za janga la Uviko-19 na ukosefu wa usalama.