1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ulinzi waimarishwa uchaguzi wa majimbo matatu Nigeria

11 Novemba 2023

Polisi nchini Nigeria imepeleka helikopta na boti za kijeshi ili kuimarisha ulinzi katika majimbo matatu yanayofanya uchaguzi wa magavana.

https://p.dw.com/p/4Yh9B
Uchaguzi Nigeria
Chaguzi za majimbo nchini Nigeria huwa na ushindani mkali na wakati mwingine hugeuka vurugu.Picha: Sunday Alamba/AP/dpa

Hatua hizo za kiusalama zimechukuliwa wakati kukiwa na hofu kuwa tofauti za kisiasa zinaweza kuzua vurugu.

Polisi nchini humo wameweka vizuizi vya safari katika majimbo ya Bayelsa, Imo na Kogi. Tume huru ya uchaguzi ya Nigeria INEC imetahadharisha kuwa haitahesabu kura katika katika maeneo yenye vurugu.

Ijumaa tume hiyo iliripoti kuwa afisa wake mmoja alitekwa nyara kwenye jimbo la Bayelsa wakati boti jingine lililokuwa limebeba nyaraka za uchaguzi lilizama, hali iliyoathiri wapigakura 5,000 jimboni humo.

Chaguzi za majimbo nchini humo huwa na ushindani mkali ambapo magavana ni watu wenye ushawishi mkubwa. Mapigano, mauaji na vitisho kwa wapiga kura vimekuwa masuala ya kawaida kwenye chaguzi za aina hiyo.