1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIndonesia

Ulinzi waimarishwa huko Papua baada ya kuzuka vurugu

24 Februari 2023

Vikosi vya usalama vya Indonesia viliimarisha ulinzi katika mji wa Wamena katika eneo la mashariki mwa Papua, baada ya watu tisa kuuawa wakati wa ghasia zilizochochewa na uvumi kwamba mtoto alitekwa nyara.

https://p.dw.com/p/4NvW9
Papua-Neuguinea | Polizei
Picha: EOIN BLACKWELL/dpa/picture alliance

Msemaji wa polisi wa jimbo la Papua, Ignatius Benny Adyolisi katika eneo hilo amesema wanausalama wapatao 200 wamepelekwa kudhibiti hali ya usalama baada ya watu 14 kujeruhiwa katika ghasia za jana Alhamisi, lakini hali bado ikiwa ni ya wasiwasi.

Ghasia katika eneo hilo zilizuka baada ya wenyeji kuvurumisha mawe kwenye kituo cha polisi cha Wamena ambapo kinamshikilia mtu anayetuhumiwa kumteka nyara mtoto wa miaka 6. Hata hivyo polisi imesema hali ya utulivu imeimarika.