1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukumbusho wa Wayahudi umezinduliwa rasmi

10 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFEs

Berlin:

Ukumbusho wa Wayahudi waliouawa na Manazi barani Ulaya umefunguliwa rasmi leo mjini Berlin. Spika wa Bunge la Ujerumani, Wolfgang Thierse, akizindua kumbukumbu hiyo mbele ya Wageni mashuhuri zaidi ya 1,500 walioalikwa kutoka duniani kote, amesema kuwa ni sehemu ya Ujerumani ya kuchukua dhamana ya maovu yaliyotokea wakati ule. Ukumbusho huo hauna lengo la kusahau yale yaliyotokea. Rais wa Baraza Kuu la Wayahudi nchini Ujerumani, Paul Spiegel, ameonya dhidi ya mahali hapo penye ukumbusho kusahauliwa katika siku zijazo. Amekosoa kuwa ukumbusho huo una waheshimu Wahanga lakini hauwataji Watesaji. Balozi wa zamani wa Israeli nchini Ujerumani, Avi Primor, amesema kuwa hakuna hata nchi moja ulimwenguni humu iliyoweka ukumbusho kwa ajili ya madhambi iliyoyafanya. Miongoni mwa walioshiriki katika sherehe hizo kusini mwa Lango la Brandenburg ni Rais Horst Köhler wa Ujerumani na Kansela Gerhard Schröder. Ukumbusho umejengwa na mchora ramani maarufu wa Kimarekani, Peter Eisenman na ina mawe maalumu 2,711 yenye urefu mbalimbali. Katikati ya mawe hayo kuna njia yenye upana wa mita moja na anayetembea katika sehemu hiyo anashikwa na hofu na kuhisi kuwa ni mpweke.