1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UKUMBUSHO WA AUSCHWITZ-ZIARA YA FISCHER WASHINGTON:

Ramadhan Ali26 Januari 2005
https://p.dw.com/p/CHOe

Dai la Kanzela Gerhard Schröder,kupiga vita barabara chuki dhidi ya wayahudi pamoja na mazungumzo ya waziri wa nje Joshka Fischer mjini Washington ndio m,ada kuu zilizowashughulisha leo wahariri wa magazeti ya Ujerumani.

Kuhusu siku ya kukombolewa kwa wafungwa wa kiyahudi katika kambi ya MANAZI ya Auschwitz miaka 60 iliopita siku kama kesho,gazeti la DIE ZEIT laandika:

"Kambi ya Auschwitz-ni jina linalowakilisha ukweli halisi wa utawala mwa kidikteta wa Ujerumani.Auschwitz inawakilisha aina mpya ya mateso ya kuwahilikisha binadamu yasio na kikomo cha wakati ambayo wanadamu waliotenda maovu hayo hawakumchelea Mungu.Kanzela Schröder alizungumzia aibu inayoselelea na aliweza kutenganisha kama walivyofanya Makanzela na marais wote wa Ujerumani kabla yeye, kati ya madhamhi ya waliotenda maovu hayo na jukumu wanalobeba vizazi vya baadae .Ukumbusho wa serikali ya Ujerumani juu ya siku hii lazima ugubikwe tangu na huzuni na hata aibu.

Kurekebisha maovu yaliotendeka,kwa uwezo wa kidunia ni vigumu.iliobaki ni kutetea haki za binadamu kila zinapokanyagwa ,kupigania pia dola zinazoheshimu sheria na uhuru kila pale palipo na umma unaokandamizwa.Siasa ya Ujerumani ijipime nguvu zake upande huo."

Ama gazeti la NORDSEE-ZEITUNG kutoka Bremerhaven laandika:

"Kutokana na historia ya yaliopita, kwetu wajerumani tunabeba jukumu kwa binadamu ambao waliangaliwa kwa jicho la kidini,kikabila au kisiasa .Kwanini jukumu hili hata wakaazi wenzetu wa kiyahudi humu nchini wanaliona kama mzigo mzito mabegani mwao,inatupasa kuliangalia kama jambo linalotutajirisha kulibeba.

Kwani katika kukabiliana na binadamu wenzetu na hasa wale wanaojikuta shidani,ndipo tunapojipima jinsi tulivyokomaa kama binadamu na tuliostaarabika." Gazeti la REUTLINGER GENERAL-ANZEIGER linatoa changamoto kwa wademokrasi wote kukaa macho kupambana na wanazi-mambo-leo.

Laandika kwamba, kwa kuwa miaka 60 tangu kutendeka madhila makubwa yasiosemeka katika ardhi ya Ujerumani Manazi-mambo-leo wanajitandaza kama walivyofanya majuzi wakati wa ukumbusho wa Holocaust katika Bunge la Mkoa wa sachsen kuonesha kibri kwa yaliopita sio tu kuhujumu desturi za yetu ya kidemokrasia ,bali pia hii ni ishara ya hatari.

Kupotoa huku historia kunabainisha kwamba ili kulind uhuru nchini humu, sio tu panahitajika wapenda wote demokrasia kukaa macho dhidi ya wachochezi hawa wapya, bali pawepo utayarifu jumla wa kukumbusha madhila waliotenda wadhalimu hawa."

Kuhusu ziara mjini Washington ya waziri wa nje wa Ujerumani Joshka Fischer , kumtembelea waziri mwenzake –mteule Bibi Condoleeza Rice, gazeti la ABENDBLATT linalochapishwa mjini Hamburg laandika:

"Kibinafsi, watu hawa wawili wanabidi kwanza kujuana. Lakini hii isionekane kama pingamizi.Ingawa waziri Fischer alikua na usuhuba mwema na mtangulizi wa Bibi Rice,Colin Powell,kisiasa lakini haikumsaidia kitu kwavile Powell hakutegewa sana sikio na rais Bush na kabisa hakuwa na ushawishi mkubwa mbele ya mawaziri wenye siasa kali katika utawala wa Bush.Kwa Bibi Condoleeza Rice hali ni tofauti.

Ni mshauri mkubwa wa chanda na pete wa rais Bush na anaangaliwa wakati huo huo kama silaha mjarabu ya Bush katika kufufua usuhuba mwema na nchi za Ulaya."

Ama FRANKFURTER ALLGEMEINE ZEITUNG linamurika tofauti ziliopo kati ya Ulaya na Marekani kuelekea Iran:

Laandika:

"Matamshi inayotoa Marekani kuhusu uwezekano wa kutumia nguvu za kijeshi dhidi ya Iran yanahatarisha diplomasia ya nchi za Ulaya .Kwahivyo, ingefaa sana kuona Ulaya na Marekani zinaafikiana juu ya msimamo mmoja jambo ambalo waziri Fischer anadai ndie shabaha yake.Kwani, ikiwa kabisa iwezekane kuizuwia Iran isiunde silaha za kinuklia,hii itayumkinika tu ikiwa pande hizo mbili zitashirikiana pamoja-shabaha ambayo anaifuata Kanzela Schröder na rais Bush aonesha kuikubali........"

Mwishoe, gazeti la OSTTHÜRINGER ZEITUNG kutoka Gera likichangia nalo katika siasa ya Marekani kuelekea Iran laandika:

"Mara hii kweli Marekani inapigania suluhishola kisiasa na kwamba vitisho vyake inavyotoa visaidie tu diplomasia ya nchi za Ulaya kufikia shabaha inayotakiwa.Lakini, iwapo mzozo wa kimataifa kama huu uko katika mikono bnarabara kwa rais Bush ni jambo la kutilia shaka shaka.Kwani, Bush haoneshi uwezo wa kushirikiana barabara na mataifa mengine.