1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine yashambulia bohari ya mafuta ya Urusi

4 Oktoba 2024

Ukraine imesema leo Ijumaa kwamba imeishambulia bohari ya mafuta ya Urusi kwa kutumia droni kwenye mkoa wa mpakani wa Voronezh.

https://p.dw.com/p/4lQR7
Urkaine | Urusi
Athari za mashambulizi ya Urusi nchini Ukraine.Picha: Wolfgang Schwan/Anadolu/picture alliance

Chanzo kimoja kutoka Idara ya Usalama wa Taifa ya Ukraine (SBU) kimeliarifu shirika la habari la AFP kwamba bohari yenye matangi 20 ya mafuta na vilainishi imelengwa usiku wa kuamkia leo. 

Taasisi zinazotoa huduma za dharura nchini Urusi ziliripoti kuzuka kwa moto kwenye eneo la ukubwa wa mita 2,000 za mraba katika mkoa wa Voronezh. 

Soma zaidi: Urusi yaishambulia mikoa 15 ya Ukraine

Hata hivyo, hapo kabla gavana wa mkoa hup alisema droni ya Ukraine ilishambulia tangi tupu la mafuta na kuzusha moto mdogo ambao ulidhibitiwa. 

Katika miezi ya karibuni, Ukraine imekuwa ikitumia droni za masafa marefu kuvilenga vituo vya nishati vya Urusi, ikisema mashambulizi hayo ni halali kwa sababu vituo hivyo vinasambaza mafuta kwa vikosi vya Moscow.